• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu, na Usimamizi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAKIKABIDHI KIKUNDI CHA BOMSATE MSAVU BODABODA 10 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 25,800,000/=..

Posted on: December 31st, 2021

MANISPAA ya Morogoro, imekabidhi Bodaboda 10 zenye thamani ya shilingi Milioni 25,800,000/= kwa Kikundi cha BOMSATE kilichopo Kata ya Mafisa Mtaa wa White House chenye Maskani yake eneo la Stendi ya Mabasi Msavu kwa lengo la kuwawezesha katika kujikwamua kiuchumi.

Tukio hilo la kukabidhi Bodaboda limefanyika Desemba 30/2021 katika eneo la Yard Magereza likishuhudiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa White House, Ndg. Said Yassin, pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mafisa, Jesca Matandura.

Akikabidhi Bodaboda hizo, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Rutahiwa John, amesema kuwa uwezeshwaji huo unatokana na fedha za makusanyo ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 ya bajeti ya Halamshauri kila mwaka kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

"Rais wetu Samia Suluhu Hassan alielekeza fedha hizi ambazo wanapewa makundi haya , zitolewe bila riba ili kila mmoja awe mnufaika, nitumie fursa hii kumpongeza Mkurugenzi wetu Ally Machela, Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kusimamia maelekezo haya vizuri na leo hii tunaona Vijana wetu wakinufaika na mpango huu, raia yangu wanapopata mkopo huu warejeshe fedha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika" Amesema Rutahiwa.

Rutahiwa, amesema kuwa katika bodaboda hizo walizopatiwa Vijana hao inakamilisha jumla ya Bodaboda 30 ambazo mpaka sasa wameshapatiwa.

Mwisho, amesema Manispaa ya Morogoro, inaendelea kuhamasisha jamii juu ya uwepo wa asilimia 10 kwa ajili ya kuwawezesha na kuinua Wananchi kiuchumi kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) ya mwaka 2020.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa White House Kata ya Mafisa ambapo kikunci hicho kipo katika eneo lake la utawala, ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Morogoro ukiongozwa na Meya, Madiwani , Mkurugenzi,pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo na watumishi kwa kuona umuhimu wa kusaidia jamii katika kuwainua kiuchumi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa BOMSATE, Awadhi Hamis, amesema mkopo walioupata watahakikisha wanautumia vizuri na kufanya marejesho kwa wakati.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA MOROGORO May 23, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA WATENDAJI WA MITAA DARAJA LA TATU TAREHE 20/6/2020 June 12, 2020
  • TANGAZO LA UCHAGUZI MKUU October 20, 2020
  • TANGAZO LA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWAN TAREHE 19.08.2021 August 18, 2021
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • RC SHIGELA AZINDUA UTOAJI WA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 5 MANISPAA YA MOROGORO

    May 19, 2022
  • KAMATI YA FEDHA MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    May 18, 2022
  • MANISPAA YA MOROGORO YAKABIDHI KOMPYUTA 30 NA PHOTOKOPI MASHINE 2 SHULE 3 ZA SEKONDARI NA VITUO VYA TRC

    May 03, 2022
  • MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MUUNGANO KWA KUFANYA USAFI

    April 26, 2022
  • Angalia Yote

Video

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MANISPAA YA MOROGORO WAZIRI KOMBO ATANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOFANYIKA NOV.24/2019.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa