Majukumu ya Idara ya maji
1. Kuratibu shughuli zote za Usanifu na Ujenzi wa Miradi mipya ya Maji Wilayani
2. Kuratibu shughuli zote za Uendeshaji na Matengenezo ya Miradi ya Maji Wilayani.
3. Kuratibu shughuli zote za Uanzishwaji wa vyombo vya Watumiaji Maji Wilayani.
4.Kushirikiana na Idara ya Mipango kuandaa Mpango na bajeti ya Idara ya Maji katika Halmashauri
5.Kusimamia Utekelezaji wa Mpango na bajeti ya Idara ya Maji katika Halmashauri
6. Kuandaa Taarifa mbalimbali za Idara ya Maji pindi zinapohitajika.
7. Kuandaa Mpango Mkakati wa Idara ya Maji(Strategic Plan)
8. Kukusanya, kuchambua na kutafsiri takwimu za hali halisi ya Upatikanaji wa Maji Wilayani.
Idara hii ina jumla ya vitengo vikuu vitatu ambavyo ni :-
Kupitia vitengo hivi Idara imeendelea kuhakikisha kuwa wakazi wa Halmashauri wanapata huduma ya maji , pia kuhakikisha kuwa wakazi wa maeneo ya pembezoni wanapata huduma ya maji kwa kusimamia na kubuni miradi mbalimbali ya maji.
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI
Idara kwa kushirikiana na wananchi, Idara imeendelea kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali katika maeneo ya pembezoni inabuniwa, kusanifiwa na kutekelezwa ili kuwapatia wakazi wa Manispaa huduma ya maji, na pia kuhakikisha kuwa miradi ambayo haitoi maji inakarabatiwa ili iweze kuendelea kutoa huduma ya maji kwa wakazi wote.
Miradi iliyotekelezwa katita kipindi kilicho pita ni Mradi wa maji wa mtaa wa Kasanga kata ya Mindu, Kiegea B Kata ya Mkundi na Misongeni, Tanki la Maji, Bomba la Zambia iliyopo kata za Bigwa na Kingolwira,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa