Mipango Miji na Mazingira:
Utangulizi:
Malengo ya Idara ya Mipangomiji na Mazingira kwa Mwaka 2013/2014 ni Malengo Matatu makubwa yafuatayo:
(a) Uongozajiwa Ukuaji wa Mji katika Misingi endelevu na ya kimkakati.
(b) Kuimarishahuduma za kiuchumi, miundombinu na mawasiliano
(c) Kuimarisha usimamizi wa Maliasili na Mazingira.
Watumishi:
Idaraya Mipangomiji na Mazingira ina jumla ya Watumishi 30. Kwa mujibu wa Ikama yaWatumishi wa Manispaa Sekta hii ina upungufu wa Watumishi 41 ambao ni AfisaMipangomiji wiwili (2), Maafisa ArdhiWaandamizi (2), Mpiga chapa wa kumbukumbu (1) na Karani Masijala WatunzaKumbukumbu 2. Wapima ardhi watatu (3), Fundi Sanifu Upimaji watano (05), Wasanifu Ramani wawili(2), Field Asst. Kumi (10), Afisa Misitu wawili (2), Wathamini Wasidizi wawili(2), Mhudumu mmoja (1) na Afisa ArdhiWasaidizi Wandamizi Wawili (2). AfisaMazingira Mmoja (1) AngaliaJedwali Na.1. Aidha kunawatumishi waliohama na waliohamia katika Manispaa hii, Angalia Jedwali na 2.
Jedwali Na. 1 – Haliya Watumishi:
NA.
|
KITENGO
|
KADA YA WATUMISHI
|
WALIOPO
|
PUNGUFU
|
1)
|
Mipangomiji
|
Afisa mipangomiji
|
3
|
2
|
2)
3) 4) 5) |
Upimaji
|
(i) Wapima ardhi
|
3
|
3
|
(ii) Fundi Sanifu na upimaji
|
3
|
5
|
||
(iii) Wasanifu Ramani
|
4
|
2
|
||
(iv) Field Asst.
|
2
|
10
|
||
6)
|
Maliasili
|
(i) Afisa Misitu
|
1
|
2
|
7)
|
|
(ii) Afisa Mazingira
|
-
|
1
|
8)
9) |
Uthamini
|
(i) Wathamini
(ii) Wathamini Wasaidizi |
3
|
-
|
1
|
2
|
|||
10)
|
Ardhi
|
Afisa Ardhi Mwandamizi
|
1
|
2
|
Afisa Ardhi Mteule
|
1
|
1
|
||
Afisa Ardhi
|
2
|
3
|
||
Afisa Ardhi W/Mwandamizi
|
2
|
2
|
||
Afisa Adhi Wasaidizi
|
2
|
2
|
||
Mpiga chapa wa Kumbukumbu
|
-
|
1
|
||
Mtunza Kumb.
|
2
|
2
|
||
Wahudumu
|
2
|
1
|
||
JUMLA KUU
|
30
|
41
|
KITENGO CHA MIPANGOMIJI:
LengoKuu la Kitengo cha Mipangomiji ni uongozaji wa ukuaji wa mji katikamisingi endelevu na ya kimkakati. Shughuli kuu zilizofanyika ni kama ifuatavyo:
Utekelezaji wa Mpango Kabambewa Manispaa ya Morogoro pamoja na Mpango wa uendelezaji Mji Kati:
Usimamizina Udhibiti wa Uendelezaji wa Mji
KITENGO CHA ARDHI
Shughuli zilizofanyika ni kama ifuatavyo:
Katika kipindi hiki, jumla yaRasimu za Hati tisini na nane (98)ziliandaliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kwa hatua za Upelekaji Wizarani kwakusainiwa na kusajiliwa. Pia kuna jumlaya maombi ya ramani ndogo za hati mia mbili kumi na tano (215) yamewasilishwa kwa ajili ya kuandaliwa na Mpima wa Manispaa
Kwa Kipindi cha Aprili hadi Juni 2014 jumla ya Miliki sabini na tisa (79) zilihamishwa kutoka mmiliki mmoja kwenda kwa mwingine nakupata kibali cha Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa.
Jumla ya malipo kwenye viwanja(132) vimethibitishwa kwa wamilikimbalimbali tayari kwa hatua za uandaaji wa Rasimu za Hati kwa wamiliki hao.
Jumla ya maombi ya Ramani zaHati (Deed Plans) 215 ziliombwa kwaMpima Ardhi wa Manispaa na kupatiwa namba (Land Office Number).
Zoezi la kuhakiki umiliki kwaajili ya utoaji wa vibali vya ujenzi ulifanyika na jumla ya Maombi (51)yalihakikiwa na kupitishwa na Ramani nne (04) kurudishwa kwa kuwa na mapungufumbalimbali yakiwemo ya miliki Pandikizina waombaji kutolipa Kodi ya Ardhi. Wananchi hao wamekuwa wakiitwa kwa barua ilikurekebisha kasoro hizo.
Kwa kipindi hiki jumla yamigogoro 15 ilipokelewa na mingine 30 ipo Mahakamani, kati ya hiyo iliyopoMahakamani migogoro 4 imepatiwa ufumbuzi/ kuamliwa katika Baraza la NArdhi naNyumba la Wilaya.
KITENGO CHA UTHAMINI
Kitengo kimeendelea na utekelezaji wa kazi zake kama ifuatavyo:
Jumlaya viwanja 60 vimefanyiwa uthamini kwa ajili ya kuandaa Hati za uhamisho wamiliki.
Wananchi 1,432 wa kaya zilizoathiriwa na utekelezaji yamiradi ya maendeleo wamefanyiwa tathmini kwa ajili ya fidia.
Jumla ya viwanja 03 vimefanyiwatathimini hiyo.
Jumlaya maombi 02 yameshughulikiwa.
KITENGO CHA UPIMAJI NA RAMANI
kitengo cha Upimaji na Ramani kiliendelea na utekelezajiwa kazi zake kama ifuatavyo:-
Kazi zilizofanyika kipindi hiki
Upimaji wa viwanja vipya:
Viwanja vinaendelea kuonyeshwamaeneo ya Kiegeya (Mangoroma UTT)na viwanja vilivyopimwa na wanafunzi wa Chuo cha Ardhi huko Kiegeya (FieldWork) kwa nguvu za wananchi wenyewe.
Utatuziwa Migogoro ya Mipaka:
Migogoro 5 tumefanikiwa kufufuamipaka kama ifuatavyo:
· Kurudishiamipaka ya viwanja namba 277 & 278 Mlimani.
· Kurudishiamipaka ya viwanja namba 3 &5 Kitalu J Kihonda.
· Kurudishiamipaka ya kiwanja namba 51 KitaluA Mji Mpya.
· Kurudishiamipaka 86/2 na 87 Kitalu A Kigurunyembe.
· Kuonyeshampaka kati ya eneo la (Mzinga Cooparation) na Kata ya Kauzeni.
· Kuonyeshaalama za viwanja mbalimbali 77maeneo ya Mkundi, Kihonda, Mazimbu, Tungi, Forest, Kichangani, Kiegeya, Lukobe,Mlimani na Kola.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa