1.Kuratibu na kutekeleza shughuli za idara Wilayani.
2. Kuishauri Halmashauri kuhusu Elimu ya Sekondari na kuweka mipango mkakati .
3. Kuandaa mipango ya maendeleo ya elimu ya Sekondari.
4.Kuhakikisha huduma mbalimbali zimetolewa shuleni kulingana na mahitaji.
5.Kusimamia utekelezaji wa sera ya elimu na Kanuni za uendeshaji wa elimu ya Sekondari.
6. Kusimamia matumizi ya fedha za Idara.
7. Kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
8. Kushirikiana na Halmashauri kuendesha semina na makongamano kuhusu ufundishaji mashuleni.
9. Kusisitiza na kushiriki katika mitihani ya mashindano.
10.Kuwatembelea walimu kwenye vituo vyao vya kazi ili kutathmini mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.
11. Kufuatilia maelekezo ya wakaguzi wa shule.
12.Kukusanya, kuhifadhi, na kutoa takwimu mbalimbali za elimu ya sekondari katika Wilaya kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya elimu.
13. Kushughulikia upatikanaji wa mali na vifaa vya shule.
14.Kutunza takwimu za huduma na matumizi ya mali na vifaa mashuleni.
15.Kudhibiti takwimu za elimu mashuleni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa