IDARA YA ELIMU MSINGI
Utangulizi:
Dira yaMaendeleo ya Tanzania ya 2025 inalenga kutokomeza kabisa umaskini ifikapo Mwaka2025, na hivyo kipaumbele kikubwa kimewekwa katika Sekta ya elimu ambayo inachukuliwa kama msingimkubwa katika kuleta mabadiliko kijamii na kiuchumi. Hivyo Halmashauri yaManispaa ya Morogoro haiko nyuma katika kudumisha Mikataba na makubaliano yaKimataifa yanayohusu upatikanaji,usawa na ubora wa Elimu.
Malengo ya Elimu:
Katika kipindihiki, Idara ya elimu ilitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sera ya elimu na Mafunzo ya Mwaka 1995 ya Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi, na Mpango wa Maendeleo ya elimu ya Msingi (MMEM) na Dira yaMaendeleo ya Tanzania 2002 – 2025 inayosisitiza kuondoa umasikini. Aidha Idarailijiwekea malengo kwa kipindi hiki kama ifuatavyo:
Hali Halisi:
Idara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi inatekelezamajukumu yake kwa ushirikiano na vitengo vyake vya (Taaluma, Vifaa na Takwimu,Elimu ya Watu Wazima (EWW), Elimu Maalum na Utamaduni. Aidha zipo Idara 2zinazojitegemea zinazofanya kazi kwa kushirikiana na Idara ya elimu Utawalaambazo ni Idara ya Ukaguzi wa Shule na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSD). PiaIdara imeshirikiana na Asasi zisizo za Kiserikali,Mashirika yaDini na Wadau mbalimbali. Kutokana na mahusiano hayo, Idara ilitekelezamajukumu yake kwa ufanisi, Idara ya elimu (Msingi) ina vitengo 4 ambavyovilitekeleza majukumu yake katika maeneo ya kielimu yafuatayo:-
Taarifa ya Elimu ya Awali:
Halmashauri ya Manispaa ina jumla ya shule 67 zenye madarasa ya awali,kati ya hizo 44 ni serikari na 23 ni shule zinazomilikiwa na watu binafsi.Shule hizo zina jumla ya wanafunzi 3638 (Jedwali Na.1).
JedwaliNa.1 - Idadi ya wanafunzi katika madarasa ya Elimu ya Awali:
Jinsi
|
Mwaka 1
|
Mwaka 2
|
Jumla
|
Wav
|
915
|
866
|
1781
|
Was
|
1010
|
847
|
1857
|
Jumla
|
1925
|
1713
|
3638
|
Chanzo – Idara ya Elimu Msingi 2014
Taarifa ya Elimu ya Msingi:
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina jumla ya shule 85 za msingi kati ya hizo shule 62 ni za Serikali na shule 23 zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi walio katika shule zamsingi ni 50,900 kati yao wavulanani 24,885 na wasichana ni 26,017.
Uandikishaji wa wanafunzi wapya wa darasala Awali na Msingi 2014
Uandikishaji wa Wanafunzi wanaoanzamadarasa ya awali na darasa la kwanza umekamilika na hali ya uandikishaji ikokama ifuatavyo;-
Jedwali 2(i) Maoteo na uandikishaji kwa madarasa ya kwanza na ya Awali
Darasa
|
Maoteo
|
Uandikishaji
|
Asilimia
|
||||
Awali
|
1342
|
1348
|
2690
|
1123
|
1197
|
2320
|
86
|
Darasa kwanza
|
3056
|
3110
|
6166
|
3011
|
3259
|
6270
|
101
|
Idadi ya wanafunzi katika shule za Msingi kwa mwaka 2014
Halmashauri ina jumla ya wanafunzi 44,676 mchanganuo upo kama ulivyo katikajedwali na 2(ii). Zoezi la ukusanyajiTakwimu za Elimu ya Msingi limefanyika kupitia maelekezo kutoka OWM-TAMISEMIkwa kutumia vitendea kazi vinavyotolewa ambavyo ni TSA (Taarifa ya Shule za Awali) na TSM(Taarifa za Shule za Msingi) vitendea kazi hivyo hupelekwa katika shule yaMsingi zote za Msingi za Serikali na Shule za binafsi.
Jedwali Na. 2(ii)- Idadi ya Wanafunzi Walio Katika Shule za Msingi zaSerikali:
S/N |
Darasa |
Idadi ya wanafunzi Wav. |
Idadi ya wanafunzi Was. |
Jumla ya wanafunzi |
1)
|
I
|
3,567 |
3,587 |
7,154 |
2)
|
II
|
3,428 |
3,432 |
6,860 |
3)
|
III
|
3,247 |
3,371 |
6,618 |
4)
|
IV
|
2,966 |
3,191 |
6,157 |
5)
|
V
|
3,181 |
3,247 |
6,428 |
6)
|
VI
|
3,035 |
3,213 |
6,248 |
7)
|
VII
|
2,413 |
2,798 |
5,211 |
|
Jumla Kuu
|
21,839 |
22,839 |
44,676 |
Chanzo: Idara ya Elimu, 2014
Jedwali Na. 2(iv)- Idadi ya Wanafunzi Walio Katika Shule za Msingi zisizo za Serikali:
S/N |
Darasa |
Idadi ya wanafunzi Wav. |
Idadi ya wanafunzi Was. |
Jumla ya wanafunzi |
1)
|
I
|
694 |
693 |
1,387 |
2)
|
II
|
549 |
561 |
1,110 |
3)
|
III
|
482 |
485 |
967 |
4)
|
IV
|
400 |
452 |
852 |
5)
|
V
|
353 |
362 |
715 |
6)
|
VI
|
295 |
340 |
635 |
7)
|
VII
|
273 |
285 |
558 |
|
Jumla Kuu
|
3,046 |
3,178 |
6,224 |
Chanzo: Idara ya Elimu, 2014
PiaHalmashauri ina jumla ya wanafunzi 786wakiwemo wavulana 432 na wasichana 354 wenye ulemavu. Shule zenyewanafunzi walemavu ni pamoja na Mafiga,Kikundi, Kilakala, Mazimbu, Mwembesongo, Kiwanja cha Ndege, Mzinga, Kihonda na Bungo
Jedwali namba 2 ( v) Mchanganuo wawanafunzi na aina ya ulemavu
Na. |
Aina ya Ulemavu |
WV |
WS |
JML |
1)
|
Viziwi
|
142 |
121 |
263 |
2)
|
Akili
|
243 |
197 |
440 |
3)
|
Uoni hafifu
|
31 |
29 |
60 |
4)
|
Viungo
|
6 |
7 |
13 |
|
Jumla
|
432 |
354 |
786 |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa