• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu, na Usimamizi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha

MKURUGENZI MANISPAA MORO, AWATAKA WAKUU WA IDARA KUWEKA MALENGO HALISI ILI KUFIKIA KIWANGO CHA JUU KATIKA UTENDAJI KAZI.

Posted on: November 20th, 2019

MKURUGENZI wa Manipsaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, leo Novemba 20, 2019, amefungua mafunzo kwa Wakuu wa Idara juu  ya uzingatiaji wa kanuni, sheria na taratibu za Utumishi wa Umma.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho , amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wakuu wa idara pamoja na kutoa huduma bora na kuzingatia miiko ya kazi na kuweka malengo halisi ya kazi ili kufikia kiwango cha juu katika utendaji wa kazi .

Amesema kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na wawezeshaji kutoka Chuo kikuu Mzumbe , hivyo amewaomba watumishi kuzingatia mafunzo hayo  muhimu kwani yanawajengea uwezo watumishi kimaadili katika kazi  zao za  kila siku.

"Tumewaandalia mafunzo haya ikiwa ni sehemu ya wajibu wangu kama mwajiri wenu wa kuwajengea uwezo ili hatimaye muweze kuongeza ufanisi wa kazi kila mmoja katika eneo lake la kazi, nyinyi ni watu muhimu sana kwenye taasisi yoyote, nawaomba mjiamini vya kutosha ,muwe familia moja." Amesema  Sheilla.

Aidha, amekipongeza Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kujitoa kwao katika ushirikiano wa mafunzo hayo pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, akisema matarajio yake ni kwamba baada ya mafunzo hayo watumishi watazingatia  vizuri miiko ya kazi na kutoa huduma bora kwa Wananchi pamoja na kutunza siri za ofisi.

Naye Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro Waziri Kombo, amesema mafunzo hayo yamehudhuriwa na jumla ya Wakuu wa idara 19 na wasaidizi 30, huku akitarajia kila mkuu wa idara na wasaidizi wake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo watatoa huduma bora kwa Wananchi wao.

Pia amesema  kuwa,mafunzo hayo yamewalenga wao kwani ndio wanaosimamia idara  hivyo amewataka wabadilike na kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt John Magufuli ya kuchapa kazi kwa bidii pamoja na kufuata misingi ya utawala bora.

" Niwaombe watumishi wenzangu, ufanyaji kazi umebadilika, Rais wetu anahitaji matokeo chanya kwa maendeleo ya Taifa,  hivyo lazima tubadilike ili kuendana na kasi yake pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa muda wa kusikiliza Wananchi na muda wa kufanya kazi zako"" Amesema Kombo

Katika hatua nyengine, Afisa Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Morogoro, Ndg. Mohamed Chamzhim,  amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa kwa  kuandaa mafunzo hayo kwani yatawajengea uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi na kutoa huduma bora ikiwamo kuzingatia miiko kazini na kuweka malengo ya kiutendaji.

 Kwa upande wa Mratibu wa Kuzuia na kudhibiti maambukizi ya Ukimwi, Manispaa ya Morogoro, Upendo Elias,   amesema wao wameyapokea mafunzo hayo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wakufunzi wa mafunzo kwani yataleta tija kubwa katika utoaji wa huduma bora.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 MANISPAA YA MOROGORO December 06, 2019
  • TANGAZO LA WANAODAIWA VIWANJA MANISPAA YA MOROGORO KUANZIA MWAKA 2005-2019 December 06, 2019
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA MOROGORO KUKUTANA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO NA KUZITATUA,UWANJA WA HOSPITALI YA RUFAA TAREHE 7/11/2019 SAA 4:00 ASUBUHI. November 05, 2019
  • MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MANISPAA YA MOROGORO TAREHE 3/08/2019 July 30, 2019
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • KAMATI YA SIASA YA CCM YAIPONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KWA UJENZI WA JENGO LA UDHIBITI UBORA WA SHULE.

    December 06, 2019
  • MOREPEO YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA WAZEE VYENYE THAMANI YA TSH MILIONI 14

    December 06, 2019
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA NCHINI-WAZIRI KAIRUKI.

    December 05, 2019
  • JUMLA YA SHILINGI MILIONI 774 KUTUMIKA KATIKA UJENZI WA MTO KIKUNDI MANISPAA YA MOROGORO

    December 05, 2019
  • Angalia Yote

Video

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MANISPAA YA MOROGORO WAZIRI KOMBO ATANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOFANYIKA NOV.24/2019.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0757-226612

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa